
Idadi ya tafsiri:
25 na zinaendelea!
Ni thamani gani masomo ya Ibada Binafsi ya Matumaini ya Kila Siku yanaleta katika maisha yako?

Amani
Matumaini ya Kila Siku huleta amani na utulivu katikati ya vurugu za maisha ya kila siku.

Furaha
Matumaini ya Kila Siku huleta raha na furaha yakikukumbusha kuhusu upendo na neema ya Mungu.

Shukrani
Matumaini ya Kila Siku huhamasisha kuwa na shukrani kwa baraka unazopata katika maisha yako na kuthamini upendo wa Mungu.

Tumaini
Matumaini ya Kila Siku huleta hisia ya matumaini na matarajio makuu, yakitoa hamasa wakati wa nyakati ngumu.

Upendo
Matumaini ya Kila Siku yanakukumbusha upendo wa Mungu na kukutia moyo uwapende wengine zaidi kwa kina.

Amini
Matumaini ya Kila Siku hujenga imani kwa Mungu na yanakuhamasisha umwamini zaidi kikamilifu katika maisha yako.

Ujasiri
Matumaini ya Kila Siku hukupatia hisia ya ujasiri na nguvu, yakikuhamasisha kukabiliana na hofu na kushinda vikwazo.

Msamaha
Matumaini ya Kila Siku yanakupa msukumo kutafuta msamaha na kutoa msamaha kwa wengine, ukiimarisha uhusiano wako na Mungu.

Kusudi
Matumaini ya Kila Siku yanakupa hali ya kuwa na kusudi na maana ya maisha yakikukumbusha kuhusu utume wako kama Mkristo.

Uhusiano
Matumaini ya Kila Siku hutoa hali ya uhusiano na Mungu na waumini wengine, yakijenga hali ya jumuiya na ya kujisikia nyumbani.
Masomo ya Ibada Binafsi ya Matumaini ya Kila Siku


Mara nyingi nimekuwa nikifikiri kwamba watu wa kipekee ni watu wa kawaida tu ambao wanajiambatisha kwenye maono ya kipekee, maono ya Mungu. Na ninashawishika kwamba hakuna kitu kingine katika maisha kitakacholeta hali ya kuhisi kujitosheleza kuliko kufanya kile ambacho Mungu alikuumba ufanye.
Ili kukutia moyo unapoelekea kufanya kile ambacho Mungu ameandaa kwa ajili yako, nilitengeneza Matumaini ya Kila Siku, masomo yangu ya ibada binafsi kwa barua pepe BILA MALUPO yanayokufikishia mafundisho ya Biblia kwenye kikasha chako kila siku. Kujiunga na Matumaini ya Kila Siku kutakupatia hamasa ya kujifunza neno la Mungu na kujenga uhusiano wa kina wenye maana pamoja naye, ambao ni jambo muhimu ili kuishi maisha uliyokusudiwa kuishi.


Matumaini ya Kila Siku ni nini?
Matumaini ya Kila Siku yamekuwa yakipeleka Neno la Mungu kupitia mafundisho ya Mchungaji Rick kwa mabilioni ya watu karibu katika kila nchi duniani tangu mwaka 2013. Unaweza kupata mafundisho ya Matumani ya Kila Siku, makala ya ibada binasi kupitia redio, programu za kijiditali (app)podkasti, video, tovuti, barua pepe, nyenzo za uanafunzi na mitandao ya kijamii (Facebook, Instagram, Pinterest, na YouTube).